Wengi wetu tumekua tukidhani kua kazi nzito ni ujenzi wa nyumba na sio finnishing,,,,naomba kuwaeleza leo kua sio kweli kwa asilimia flani........
Jamani finnishing ya nyumba ni gharama kuliko ujenzi....tutambue hilo, na utakuta wengine mpaka miaka kadhaa hawajamaliza, kwa kua wanajua nini wanafanya ...
Kinachohitajika ni kujipanga, na kutafuta mtaalam aweze kukusaidia katika hili....unaweza kujenga nyumba yako vizuri...lakini ukija kwenye finnishing unaanza kubania hela na kutaka virahisi...yaani jua kua nyumba unaiharibu na hutokua umefanya kazi yoyote ile......nyumba itakua mbaya mbaya na unaweza kujuta.....
Tujitahidi katika hili kua kama najenga nyumba yangu basi ni afadhali nifanye taratibu kwa ufasaha kuliko haaraka haraka na ukaharibu kazi......
Tujitahidi kua wavumilivu katika kumaliza nyumba zetu kuliko haraka haraka, ninasema hivyo kwa kua nakutana na watu kama hawa, na kwa kweli katika kazi yangu sipendi haraka ya kupitiliza kabisaaaaa.......
Kazi ya designing inahitaji muda na nafasi. bila hivyo ni kuharibu kazi.....nami sipendi hilo litokeeee....
Kwa kwetu Tanzania bado tuko nyuma katika hili ingawa tunajikongoja na tutafika kwa kuelimishana na kuelewana...