Thursday, August 12, 2010

KUPIGA PICHA KABLA NA BAADA YA KAZI NA KUJA KU SHARE NA WADAU WENZETU

Dear all, napenda kuchukua fursa hii kutoa somo kidogo kuhusu kupiga picha za before and after za kazi zangu.

Dhumuni ya kupiga picha ni kuonyesha ni jinsi gani tunaweza ku share aidia na wenzetu, na kuendelea kuelimishana juu ya hili. 

Kama kila mtu angekua anakataa kupiga picha kazi aliyofanyiwa tuwengeweza kweli hata ku download kwenye internet? Na hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wamekua wakiendelea, maana hawakai na mawazo ya maendeleo wao binafsi

Homez Deco Kreative Homez, inapomfanyia kazi mteja wake inahakikisha ameridhika, na hua tunapiga picha kabla ya kuanza kazi na baada ya kumaliza kazi. Na hua tunataja tuu mahali ya sehemu kazi ilipofanyika, tunajua kua kuna mambo ya uhalifu etc. yote hayo tumezingatia na ndio maana hatutoi details za mteja zaidi ya kutaja mkoa.

Nawaomba ndugu wadau, muondoe wasiwasi, woga etc, ili tuendelee kuelimisha, maana ndio lengo la blog hii na si vinginevyo kama baadhi ya wengine wanaoanza kuibadilisha lengo la blog hii iwe uwanja wa malumbano.

Kama una mawazo, mchango, ama hata kama umedecorate mwenyewe nyumba, chumba, sehemu ya biashara, garden etc. Piga picha ututumie nasi tuuta share nawe na kusaidiana katika hili.

Nimekuwa pia nipigiwa simu na kuulizwa maswali ya wale wanaotaka ku decorate nyumba zao, na nimekuwa nikiwajibu bila hata charges zozote zile. 

Tuondoe wasiwasi na tushirikiane katika hili. 

Nawashukuru woote.

No comments:

Post a Comment