Friday, May 9, 2014

USAFI WA MILANGO YA MBELE YA NYUMBA ZETU.Asilimia kubwa ya nyumba za Kitanzania milango ya mbele ya nyumba zetu hua hatuitumii....yaani labda mgeni kaja...au labda tunataka kuiniza vitu ndani ndio tunatumia huo mlango.

Asilimia kubwa hua tu atumia mlango wa nyuma ambao ni wa jikoni...


Sasa basi naomba tukumbushane swala la usafi wa mlango wa mbele...hata kama hauutumii jamani mlango huu unahitaji kua msafi muda wote...


Unapofanya usafi sitting room fungua na mlango huo  ufanye usafi pia...

Haileti maana eti mlango unafanyiwa usafi mara chache kisa hautumiki ama mpaka mgeni aje au unataka kuingiza vitu  ndio ufanyiwe usafi.

Nyumba inatakiwa kua safi muda wote...wakati wowote...kwa afya yetu na kwa muonekano safi....tuwe tunawakumbusha na kukagua wadada wa kazi ama wasaidizi wetu na maramojamoja uwe unatokea mlango wa mbele hii itakusaidia kukagua na kujenga mazoea ya kufanya usafi eneo hili.


No comments:

Post a Comment