Friday, February 22, 2013

For Sale items....


Habari wadau,

Baada ya ukimya kidogo kwenye blog, ambao ni kwa ajili ya kazi, za kwenda site......

Leo ninakuja kwenu na mada ya kuuza vitu vya ndani ambavyo hamvitumii, ama mnataka kubadilisha, mtoe vya zamani mlete vipya...

 Iwe ni majumbani ama ofisini, iwe ni vya garden ama garage

Sasa basi vitu hivi mnaviweka wapi? ama mnafanya navyo nini?

Huku ninakotembea, hili swala ninakutana nalo, naniongea na wadau, na ninashukuru kwamba wanaliitikia, na naona tunaanza kutoa vitu vyetu na kuviuza, kwa bei ambayo ni reasonable, na hata wewe muuzaji utapata hela ya kufanyia kitu kingine.....

Utakuta vitu ni viko katika hali nzuri mtu kavijaza ndani, ama kaweka stoo, ili mradi tuu ni vurugu....nyumba imejaa, hakuna nafasi, vitu vimesongamana....na bado analeta vingine...

Hivi unajua kua kabla ya kwenda kununua kitu lazima ukitafutie sehemu ya kukaa kwanza ndio ukanunue....

Nawaomba watanzania wenzangu, kwenye suala la ku pamba nyumba zetu hili nalo lipo.....la kupunguza vitu ndani, kabla ya ku anza kupamba.....Vitu vingi vikijaa ni uchafu, nasio kwamba ndio nyumba imekua ya kisasa.....kwa kujaza vitu.....

Chochote ulichonacho, na ambacho haukitumii...tuko sisi tunaweza kukitumia ni wewe kuamua kukitoa....

Homez Deco tumejitolea kukusaidia kuviuza vitu vyako kwa kutanga kwenye blog yetu, na wadau wavione na waweze kununua. kwa watakaohitaji...

Kuliko kukaa na kitu, mpaka kinaharibikia stoo.....na kuendelea kueleta msongamano wa vitu ndani...

Vitu hivi vinaweza kua ni fanicha yoyote ile, iwe ni ya ofisini ama nyumbani...

Na visiwe vimechoka sanaaaa ama vimechakaa sana......viwe katika hali nzuri....maana Homez Deco kabla ya kuviweka kwenye blog ni lazima tuviangalie...

Utahitajika kututumia picha ya kila upande  wa kitu hicho unachotaka kukiuza....

Zoezi hili ni kwa yoyote yule...iwe ni Dar ama mikoani.....Tuwasiliane kwa email; sylvianamoyo@yahoo.com ama simu: 0713 - 920565.....


1 comment:

  1. Asante sana, Sylvia. Ni wazo zuri na mbinu bora ya kuokoa pesa na kuleta nafasi ndani ya nyumba!

    ReplyDelete