Pamoja na Miji mikubwa ya nchi yetu, nawaombeni wa dau wa mazingira popote mlipo mwaka huu uwe wa usafi, ktk miji yetu, makazi, maeneo ya kibihashara, mpaka majumbani mwenu mnapoishi, tulipe kipaumbele kwa ujumla suala la uhifadhi wa mazingira acheni kutupa taka hovyo,, kwenye vijito vya maji,chini ya madaraja, barabarani acheni kutupa taka ovyo kwa ujumla, utakuta sehemu kuna garage ya magari na pembeni kuna mama ntilie. hivi sisi ni vipofu?? moshi wa magari harufu za desel na petrolium zote zinaelekea kwenye vyakula ambavyo mnakula.
Jamani hili nalo mpaka serikali itangaze kila mtu awe askari na mlinzi wa afya yake, na mazingira yanayowazunguka, inasikitisha sana baadhi ya maeneo ya jiji la Dar uchafu ulivyotanda kila kona halafu wakazi wa hayo maeneo hawana hata habari, kuna baadhi watu ukiona maeneo wanayoishi, na familia zao ni hatari tupu, mfumuko wa magonjwa ya milipuko, unazidi kuongeka.
Kuna reseaches ambazo zimefanyika, ktk university mbalimbali hapo USA zinaonyesha kabisaa baadhi ya cancer zinatokana na, moshi wa magari, ambayo yanatumia petrol au desel ambazo zina madini ya risasi hii ni hatari sana, kwa sisi wote, Ndio maana kipindi fulani serikali ilipika marufuku, kuweka mafuta ukiwa na abiria ndani ya basi hii ni hatari sana, hili ni jukumu la kila abiria kukataa hichi kitu . wapendwa naomba niwaambie unaweza kununua spear parts za magari popote pale ila spear parts za mwili hazipo?
Chunga afya yako, hayo masuala yote yanahusiana na mazingira, yanayotuzunguka, kiwango cha cancer nchini kimekuwa kikubwa sana inatokana na, maendeleo ya viwanda, magari machakavu, vyakula ambayo si vya asili, organic foods ambavyo baadhi ya wanajamii wanoishi mjini wanakula sana vyakula vya makopo siyo salama kiafya na usafi wa vyakula kama mboga mboga matunda ambavyo vinauzwa kwenye mazingira ya uchafu,tubadilike kwanini ule chakula cha baridi?
kwanini ununue juices ambazo zimezungukwa na mainzi kila kona?? kwanini ununue nyama butchers ambazo siyo safi na wanakufungia kwenye magazeti ambayo, yamekuwa printed na chemicals, hakuna kitu kinachoniuzi kama kufunga, chapati au maandazi kwenye magazeti ni uchafu pia kwanini usiende na mfuko wako au kifaa chako
jamani haya yote ni chanzo cha cancer na wale wenye mazoea ya kuweka chips kwenye plastics bags acheni ni cancer mnanunua mwenye cancer, chochote kile cha moto hasa chakula ukiweka kwenye plastic bags, kuna chemical fulani kwenye hiyo mifuko zinategeneza aina fulani ya vimelea vya cance, hii ni juu yako wewe mtumiaji.
Quit using it or pay later is up you all, everyone is responsible for your own health, nadhani mmenielewa mungu awalinde na tuanze mwaka huu, vizuri na malengo yetu yatimie mungu awabariki sana,
From Jossyanne - USA
No comments:
Post a Comment