Friday, May 11, 2012

Maandalizi ya Website yakiendelea......

Mambo ya mtandao, sasa hatutembei na files za catalogue, ni kitu cha ipad hapa......Thanks Lord naendelea kupiga hatua taratibu kwa juhudi zangu mwenyewe......I love my self




Huyu ndie aliyewezesha website yangu mpaka iko hewani, na yeye ndie atakua akihusika na maswala yote ya website, isiende kombo.........ni web designer......sio kwamba ninamsifu, ila katika kutafuta web designer wa kunifanyia kazi yangu hii, nikakutana nae, tena nilimpata kwa mteja wangu mmoja ndio akaniunganisha nae. Anaitwa Kaduma huyu web designer wangu.

Yaani this guy, anajua anachokifanya, na anajua kazi yake, hana haraka haraka ya kufanya kazi bora liende tuu... ana anafanya kazi kulingana na wewe unachokitaka na anakupa ushauri, na hakatai mawazo. Na imetuchukua kama miezi 2-3 hivi, maana tulikua tukiiandaa na kupumzika na kutafuta hela... hhahha si unajua tena tunajikongoja... hahaa.... lakini hakuchoka wala kukasirika. etc..... kwa ufupi he is a great guy of all.......atakaemhitaji contacts zake ziko hapo juu kwenye tangazo.......then utakuja kuniambia.....


hahahaha, imetokea wote leo tumevaa blue..... hhahahaha.... ila tumependeza ehehehhe hahahaah

Bado tunaendelea na kuijazia sehemu ambazo zinahitajikaa, maana ninataka iwe ni directory ya Interior decorations, etc...... sasa jamani si kazi ndogo hii naomba tuwe tunavumiliana pale ambapo ninachelewa ku post, ingawa sitakua ninakaa muda sana..... na hii ni kwa ajili yenu ndugu watanzania wenzangu, ninataka ifike mahala sasa, unahitaji kitu basi wewe unaingia kwenye website na blog yangu na kutafuta kampuni unazozitaka, na kwenda kwenye website zao.... na hii naona itasaidia sana sana, wawe wana update website zao mara kwa mara kwa kuweka vitu vipya walivyoagiza.

Natumai kwa kufanya hivi jamani tutakua tunaokoa muda, maana kwa sasa unahitaji kitu nahujui wapi pa kukipata, mwishowe hela unakula.......

Kwa kusema ukweli hii kazi ni ngumu, maana ni mpaka makampuni yaelewe na wanikubalie, sasa sio kazi ya leo ama kesho kukubaliwa, ila ninaamini nikiianza mapema itakua rahisi kwetu wote sote...

Ninajaribu kuwapa mawazo yangu ya nini nafikiria kukifanya na wapi tunakwenda, ninahitaji ushirikiano wenu wa hali na mali, kwa kunivumilia ili tufikie malengo.....ifike pahala na sie tunaweza kununua vitu online kwenye makampuni yetu ya nchi yetu hii.......najua inawezekana na ndio maana ninataka kuifanyia kazi......

Jamani kuna watu wamekaa tuu na kutafuta mawazo ya watu na wao waige ili watoke....... naomba kusema kua sitoogopa, wala kumuonea mtu huruma, nikiona mtu kaiga haya mawazo yangu na kuyafanyia kazi........yaani nitamuaibisha mpaka atashangaaaa, na nadhani kwa hili ndugu wadau tutasadiana na watu wa namna hiiiii.

Kwa haya mafupi napenda kuwashukuru wote kwa kuendelea kua nami na mnaendelea kua nami maana bila ninyi nisingefika hapa nilipo na kujivunia kazi yangu......naendelea kuomba mawazo yenu juu ya hi website yetu, kama kuna kitu tuongeze, tupunguze, etc.... nitayapokea na kuyafanyia kazi....

Nawatakia weekend njema.......



9 comments:

  1. Big up girl!! God bless the work of your hands!!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana mimi ni mpenzi wa blog yako tunashukuru kwa kweli unajitahidi sana kutuletea mambo mazuri.

    Pili nilikuwa nasema uoni mtu akichukuwa ideas yako ni nzuri sababu km ingekuwa mbaya hasingechukuwa sithani issue ya decoration umezaliwanayo i believe kuwa na wewe uliona sehemu ndio ukaiga na kufanya maamuzi ya kuanzisha. yangu ni hayo tu kwa kweli.Mnatakiwa mpendane.

    ReplyDelete
  3. hey hongela sana
    ulicho andika ur total wrong wewe unajua kunamtu ananifanyia kazi zangu tangu 2007 na aliweka blog yake nadani 2009 ila nahisi alikuwa na matatizo kidogo akawa ablog ila anafanya shuguri hizo she is good na kaziyake na makini sana tuuu akianza kublog ntakwambia ufungue blog yake angalie pic aliweka useme nani kaiba lini harafusasa usiseme mtu kuniiga sjui nini hapana bwana duniani tubo ma bilion a mabilio so dont think that ur too smart kuwaza
    vitu kunawaliowaza kabla ujazaliwa labda so acha izoo,,,,, ila hongera

    ReplyDelete
  4. umesema unaandaa directory? nilikuta hii website, labda itakupa some ideas, http://www.decorpad.com/index.htm

    sijaelewa exactly umemaanisha context gani ya mtu kuchukua idea yako, ila nakubaliana na mdau hapo juu, it's a blessing in disguise. Naelewa jinsi gani inauma na kukatisha tamaa.....ila pia inategemea, kama ni kuweka kwenye blog/gazeti (media), then anatakiwa aandike the source, ila kwa field uliyopo, nadhani unaelewa kuwa si wote tunaweza kuafford the price of your items, kwa hiyo kama mtu akiona design akaipenda then mkashindwana bei, sidhani kama unaweza kumzuia asiende kwa mtu mwingine akatengenezewa the same thing at a much cheaper price, pia kwa watu wa mikoani sidhani kama watakuja ofisini kwako

    mie nadhani lengo lako si tu kufanya biashara ila kutusaidia wote toboreshe nyumba zetu na kuzipenda zaidi

    kila la heri dear, tupo pamoja

    ReplyDelete
  5. Hi wadau, kwanza nashukuru sana sana, na nimefurahi na najua kua tuko pamoja, unajua hataka kama mtu akianzisha blog yake miaka kumi iliyopita ya decor, mie sina tatizo, kabisha na ningependa tuwe wengi kwani soko bado ni kubwa na mimi mwenyewe siwezi kulihimili katika hali ya kibinadamu,

    Nilichomaanisha ni kwamba tukubaliane tu kua kuna watu wanaiba aidia za wenzao, baada ya kuzisema in public ndio wanazifanyia kazi, siku zote walikua wapi kuzifanya? Sasa ndio utaona watakavyo anza kuzifanyia kazi...ninajiamini na ninachokifanya, napenda kazi yangu, mimi kama mimi nimejitolea tuelimishane watanzania wenzangu, na sijakataza wala sitokataza watu kuchukua designs na kuzitengeneza huko waliko, kua na amani tuu kutafuta mahala ambapo utaona unaweza ku afford kutengenezewa unachokihitaji, ndio maana ya hii blog.

    Nitakachokifanya ni kuwarahisishia ninyi ndugu zangu......na nitajitahidi kila niwezalo tuweze kusaidiana kwa hili......

    Kuanzisha blog si kazi, Maintaining a blog it's not a joke........

    Nadhani nimeeleweka tuuu, sikua na nia mbaya kama baadhi yenu mlivyofikiria. Napenda kukosolewa, kushauriwa, etc.....bila nyie nisingekua hapa......

    ReplyDelete
  6. I know that guy,we went school togeth. He is multiskills...............lols

    ReplyDelete
  7. Kuchukulia ideas ni kawaida usikasilike mama wote wanaiba tu.

    ReplyDelete
  8. Hi dear, hongera kazi, nzuri, usiogope competitors, kwani sisi wateja tunajua tunataka nini na wapi kinapatikana, kwanza ndio itakufanya ukue zaidi ya hapo.Remain Blessed

    ReplyDelete