1. Uwe na plan iliyo kamilika:
Ukiwa na plan iliyokamilika, ya nini unataka unaweza ukapanga uanzie wapi, na kwa awamu. Hii itakusaidia, kuepuka ama kupunguza makosa ya kuweka vitu kimakosa, kama switch etc.
2. Floor plan yako iliyokamilika ni nzuri kwa kuanzia:
floor plan nzuri na iliyokamilika inakusaidia kujua ukubwa wa sehemu yako na vipi utapangilia furnitures zako kwa size na bila ya kua na mlundikano wa vitu ndani.
3. Uchaguzi wa taa, switch, sockets etc. ni uamuzi mzuri:
Ipi inakwenda wapi, na inakaa wapi, inatakiwa ijulikane kabla ya yote, na mpangilio mzuri wa taa unahitajika angalau kwa njia 2 ama 3 za switches. Na pia, katika kundi hili kuna sockets za simu, computers,pasi etc. zote ziwe kwa mpangilio mzuri.
4. Uchaguzi wa rangi ni rahisi kupatia nani rahisi kukosea:
Kupaka rangi kwanza sio chaguo zuri kwa kuanzia, rangi zina tabia ya kukufanya ujisikie vizuri ama vibaya kulingana na ulivyozichanganya, Ushauri wa Interior decorator ama designer, utakusaidia sana kufanya asubuhi yako kua nzuri, na jioni yako kua ya mapumziko.
5. Style hubadilika:
Style sio tuu iko kwenye muonekano, lakini hata pia kwa ajili ya jengo, na pia ni muhimu kwenye project yako hii na kukufanya uwe makini kwenye hii project yako.
6. Kua na imani na subcontractors:
Subcontractors unaowachakua ndio mwangaza wa project yako, na hakikisha wanafanya kazi ontime, wanafanya vizuri, sio wababaishaji na wawe na uzoefu wa kutosha, usipokua makini, project yako hii inaweza ikawa ni mojawapo ya ndoto mbaya siku zote.......
7. Kila mtu ajue:
Ni vizuri mwenzio ajue (Husband or Wife) nini unataka kufanya na mkubaliane, ili kuepuka kurudia vitu mara mbili mbili,
8. Picha za ukutani:
Pata ushauri wa jinsi gani ya kutundika picha zako za ukutani, kutoka kwa professionals, na itakusaidia kua kila kitu kinakwenda kwa mpangilio, na kupendeza.
9. Mapambo:
Mapambo sio rahisi kama tufikiriavyo, maana hii ni kitu muhimu sana kwenye project yako, Kua na uchaguzi mzuri wa mapambo ni kama vile vile unavyopanga hii project, bila kuidharau. Hii ni hatua ya mwisho na inatakiwa ipendezeshe na sio kuchukiza, ama kukaraisha. Jaribu kwenda taratibu na kila pambo, ina hii itakusaidia kutokua na vitu viwili viwili, na kuharibu budget.
10. Landscaping/garden:
Hii ni kama nguo, yaani ni muonekano wa kwanza kwenye nyumba yako. Muonekano wa nyumba yako kwa nje siku zote unatakiwa kua mzuri, msafi , wakuridhisha na ulioko kwenye mpangilio mzuri. Ni viziru kua na plan ya garden yako kabla haujaianza ama kuanza kununua maua etc. Utakapokua na plan yako na umeridhika nayo sasa, anza kuangilia systems za maji, kabla ya kuweka udongo, mbolea etc. Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea na kuanza kuifanyia kazi kwa kupanda etc.
11. Fengshui:
FengShui is a Chinese Science that has to do with the energy in your house and office. Their basic principles are that the good energy is running very smoothly all around your place. A good combination of fengshue and a good design can be a great asset.
Today in the western hemisphere you will find many interior designers and architects that naturally incorporate these basics in their projects. (nitaielezea zaidi kipengele hiki)
12. Vitu vya kuzingatia kwanza.
Nafasi, ceiling, kabati ya nguo, milango, taa, sauti, jikoni, sakafu, rangi, pazia, garden, picha za ukutani, ukuta.
No comments:
Post a Comment