Homez Deco imeona ni vema kuanza kuangalia chumba kimoja kimoja katika upande wa mapambo kwa kadri ya uwezo wa mtu mwenyewe.....
Kuna kama makundi matatu hivi kwa upande wa kupamba nyumba zao....
Kundi la kwanza ni jamii ya Waarabu:
Mtakubaliana nami kundi hili la kwanza wao hupenda sana nyumba zao, kwa mapambo na hua ni mara kwa mara huzipamba.......
Kundi la pili ni wale wote wanaopamba nyumba ikikaribia sikukuu:
Kundi hili la pili lenyewe ni mpaka sikukuu ikaribie ndio nyumba zipambwe, na ikisha sikukuu basi inasubiriwa ingine.....
Kundi la mwisho ni wale wanaopamba kwa msimu......
Hili la mwisho wao ni kwa msimu, yaweza kua ni kila baada ya miezi 3 ama miezi 6 ndio wanapamba nyumba zao......
Ila pia haijalishi wewe ni kundi gani, maana pia tunaangalia na mifuko inachangia na hulka ya mtu pia.
Zifuatazo ni baadhi ya dondoo za upambaji wa sitting room yako:
1. Ndugu mdau, unaweza ukaanza kuanza kwa kuangalia sitting room yako imekosa nini ama inahitaji kitu gani kabla hata ya kuanza kufanyia kazi.......je ukuta rangi yake inaridhisha, ama makochi yanahitaji kubadilishwa kitambaa au kusafishwa, ama kununuliwa mengine, ama pazia ziwe zingine, je sakafu yako iko nzuri, carpets, meza ya tv, taa, cyling board.etc
2. Baada ya kujua nini utahitaji kukifanya, unaweza kumtafuta mtaalamu wa kupamba nyumba ama ndio uanze kuzunguka madukani, ama kwenye websites/blogs za mambo ya decorations za majumbani na uweze kujua vitu vipya vinavyokwenda na wakati, na kipi umekipenda na kujua pia bei za vitu hivyo....hii itakusaidia kupanga budget yako na urembe sitting room yako kwa budget.
3. Kama ulimuingiza mtaalam kazi itakua rahisi, na hutopata stress, maana pia atakushauri ni nini cha kufanya katika sitting room yako iweze kupendeza.
4. Nunua vifaa vinavyohitajika, kama uliamua kupaka rangi ya ukuta, ama kama uliamua kubadilisha kitambaa cha makochi, ama uliamua kushona pazia mpya, na hata kununua mapambo ya ndani kwako......
5. Ningependa kusisitiza kua, kama unavitu vya kupunguza ndani katika sitting room yako, kama vimechakaa, ama umevichoka, etc....huu ndio wakati wake, haina haja wala maana ya kuendelea kukaa na vitu usivyovitumia maana vinajaza sana sanaa. sitting room yako bila maana yoyote ile......
6. Na itakapo kua imefika muda wa kufanya marekebisho na kupamba...basi kazi ianze na utajikuta kua kazi inamalizika mapema, na bila kuumiza kichwa chako ama kukuchosha......
Mwisho, utasherehekea sikukuu yako ukiwa na amani, na sitting room yako ikiwa safi na nzuri ya kuvutia...
Hizi ni baadhi tuu ya designs za sitting room......
design kama hiyo gharama yake inaweza kua ni ngapi??? i mean the same design as shown in the pictures...
ReplyDelete