Thursday, July 4, 2013

JINSI YA KUWEKA FLAT SCREEN UKUTANI BILA NYAYA KUONEKANA......


Nakumbuka kuna siku niliwaambia kua nitawaletea makala ya jinsi ya kuweka flat screen ukutani bila nyaya kuonekana.....
Hili limekua ni tatizo kubwa miongoni mwetu, maana utakuta nyumba nzuri, sitting room nzuri ila kwenye ukuta wa tv nyaya kibao kiasi kwamba sasa inaharibu muonekano na kua kama uchafu.....

Wengi wetu, kwenye upande wa tv hua tunachukulia tuu ni rahisi kuiweka juu ya meza ama ukutani kwa kua ni flat tv basi haina neno, na tunasahau kabisa swala la nyaya zake kuonekana......Katika picha hizi hapo chini zinatuonyesha ni jinsi gani ya kuweka tv zetu ukutani kwa usafi.......

Maana tunajiuliza maswali mbona ukiangalia picha za wenzetu, wao tv zao zinakaa kiusafi...bila nyaya kuonekana? Jibu ni hili



 Kwa wenzetu, nyumba nyingi wanafanya partition, za mbao na  boards etc.....na zinakua na finnishing nzuri na huwezi jua kama ni partition.....hivyo inakua ni rahisi hata kutoboa na kurekebisha etc......

Sasa basi hata kwetu inawezekana, kama ndio unataka kuanza ujenzi, basi fuatilia katika hapa na mwambie archtech wako ama interior desiger wako kua hutaki nyaya zionekane na muanze maandalizi ya kuficha nyaya......Ukitumia wataalam inakua ni rahisi kwako kua na nyumba nzuri na ya kisasa......
 Wengi wetu hua hatutumii interior designers, ama tumekua tukiona gharama, ama hatutilii maanani katika swala hili...na mwisho wa siku unakuta nyumba imesha na haina mvuto....na kumbuka umetumia hela nyingi katika hili......

 Huu ndio muuonekano wa tv zetu katika nyumba zetu........sidhani kama kuna atakaebisha hapa, ...yaani kwanza ni hatari, na kunakua ni kuchafu.
 Muonekano huu ndio unaotakiwa katika nyumba zetu......haya na tuanze maandalizi ya kupachika flat screen ukutani....

 Toa Tv yako ukutani, na ama iweke chini kwa uangalifu mkubwa, ama weka kwenye kochi, ama sehemu nzuri ili isije kuvunjika....na kama ni chiki basi walau kwenye carpet ama ongezea vitu ili upate pa kuiweka kwa muda........
 Chukua ile hanger ya tv ya ukutani, na upime kisha toboa katika zile alama ulizoziweka.kwa kutumia drill maana hua inatoboa kwa usafi.....

 Hii ndio hanger ya ukutani ya tv, hua zinauzwa na tv zake....ingawa kwa huku hua wanazitenganisha.....si unajua ki TZ TZ tena........
 Ukiangalia nyuma ya tv yako kuna scruu 4, fungua na uweke ile handle ya hanger na ufunge kwa umakini.....
 Baada ya hapo, funga hanger yako ukutani, na hakikisha kua imesha kaza vizuri, maana isije kudondoka siku.
 Sasa kwa kua ukuta wetu ni board, basi toboa kwa kitu cha ncha kali kwenye lile tundu katikati......hili ndio maana yakekua nyaya zipitie hapo....
 Baada ya hapo pima kwa kwenda chini, na utoboe tena, ila sasa angalia tundu hilo la pili, lisionekane, yaani ukatoboa juu juu, itakua ni uchafu tena....

 Umeweka alama yako, sasa toboa,......

 Hapa sasa unaweza kutumia kitu utakachoona kinafaa kuingizia waya kuanzia juu ya lile tundu la mwanzo na kutokea tundu la pili chini.....
 Siku zote kwenye kuweka na kupima level, tunatumia hii ruler inaitwa pima maji kwa kiswahili cha kiufundi....hii inakusaidia kuona kwamba imekaa level........
 Ingiza nyaya zako kuanzia juu kuja chini.......na huu ndio muonekano wa nyaya zilivyoingia....

 haya nyaya zako pia uziingize zikiwa zimefungwa vizuri zisije kukaa vibaya tena huko ndani.......

 Na huu ndio muonekano wa tv yako ambayo tayari tumeshaingiza nyaya na hazionekani. Nyumba ya tv hakuna nyaya.
Na kwa mbele pia hakuna nyaya...yaani mtu ukikaa sitting room mpaka unatamani kuendelea kukaa na kungalia tv yako...........

Si kumependeza jamani....................

Sasa hawa ni kwa wale walioweka boards ndio utapata muonekano huu....kama huna unaweza kuweka na kukapendeza, hakuna gharama......na kama unao basi tundika tv yako...na kumbuka usiiweka tv juuu sana....inatakiwa kua eye level.........

Nitaleta tena somo kwa wale wenye ukuta.....jinsi ya kutundika ftat tv ukutani bila nyaya kuonekana.....


NB:
Kwa mahitaji ya kuwekewa hii board, ili tv yako ikae vizuri wasiliana nasi tutakuwekea......Haijalishi kama ni nyumba ya kupanga ama ya kwako...zote zinatakiwa kupendezaaaaaa.....si ndiko unakoishi.....ndio kwako hapo.........na ukuta huo unaweza kuupaka rangi iliyokolea...ama bold color...maana ndio focal point yako hiyooooo......

Picha kwa niaba ya house of hepworths.

No comments:

Post a Comment