Tuesday, June 18, 2013

PRIMARY COLORS

Niliahidi kutoa somo la rangi wiki zilizopita, ila kwa bahati mbaya tukawa tumepata tatizo la internet.





Sasa basi katika somo la rangi nimeona nianze mwanzo kabisa....ili liweze kutusaidia, na tuweze kujua utumiaji wa rangi, na rangi zipi zitumike wapi na kwa muendelezo upi ili upate mandhari ipi na ulioikusudia.

Primary Colors.....

Primary colors ziko tatu, ambazo ni Nyekundu, Bluu na Njano.  Rangi hizi zimepewa jina hilo kwa sababu zinajitegemea nani rangi za mwanzo kwa upatikanaji wa rangi...haziwezi kutengenezwa kwa kutumia rangi zingine zikatokea hizi primary colors...Nikiwa na maana huwezi kuchanganya rangi flani na flani ukapata njano ama blue ama nyekundu.....

Rangi hizi ndio kianzio cha kupatikana  rangi zingine kwa kuchanganya rangi mbili tofauti katika hili kundi la primary colors. Hua tunaziita pigments.

Mchanganyiko huo wa rangi  mbili ndio unaofanya rangi kuvutia, na kupata rangi uliyoikusudia, ikichanganywa kwa uangalifu na kwa kiasi kinachohitajika.

Kwa mfano kupata rangi za nyumba, za wachoraji etc.....lazima watumie primary colors ili kuweza kupata rangi zingine na ambazo wamezikusudia......

Somo litaendelea........



No comments:

Post a Comment