Monday, October 29, 2012

Uzuri wa sebule......





Angalia picha hizi na uone uzuri uko wapi wa hizi sebule. Je ni lazima uwe na fanicha za gharama ndio sebule iwe nzuri, ama ni mpaka vitu vijazane ndio sebule iwe nzuri. ama ni nini haswa hufanya sebule kua nzuri.....

Kwa muono wako wewe unaonaje?

Ukiniuliza mimi jibu ni kwamba, haijalishi eti mpaka uwe na fanicha za gharama, ama ujaze sebule. n.k. hapana. Sebule yako hiyo hiyo uliyo nayo, ukiibadilisha kwa kupunguza fanicha zilizojana ili uweze kupata nafasi, ama kuongeza vitu kidogo kwa sebule iliyo pwaya , ama kwa kubadilisha zulia lako kama limechakaa, badilisha kitambaa cha sofa pia kama kimechakaa (kama bado unalipenda sofa lako), bila kusahau rangi za ukuta pia, paka rangi kulingana na ukubwa wa sebule yako na fanicha zilizomo kumbuka rangi zenye giza hufanya chumba kuonekana kidogo, na zenye mwanga hufanya chumba kuonekana kikubwa......

Weka picha za ukutani, hapa haijalishi kama ni za familia ama urembo... ila tuu ziwe kwenye mpangilio mzuri na uwiano mzuri unaoendana....

Usafi wa mara kwa mara pia huhitajika.....

Bila kusahau upande wa pazia, mapambo kama mito, maua, taa, etc...

Hapa sasa utakua umepata muonekano mzuri  wa sebule yako........

1 comment:

  1. Hi Silvia

    Hongera kwa kazi nzuri, wewe ni jembe mwanangu, nakukubali mdada, big up saaana. Sasa nataka kubadilisha kitambaa cha sofa vipi nije kwa ofisi yako? Au naweza pata kitu kama cha kuvalisha kwenye hayo masofa kuwa na muonekano tofauti tofauti? Naomba kujuzwa tafadhali.

    Mary wa kimara

    ReplyDelete