Thursday, May 3, 2012

Kazi ya Homez Deco-Kreative Homez, Site- Mbezi Beach.....











Ni vitanda vya four poster, design 2 tofauti, na wengi wenu mmekua na maswali kua vitanda hivi vinakuaje na je kama ni imara, jibu ni kua vitanda ni imara tena kuliko mbao, maana mbao asilimia kubwa zinaliwa na wadudu;
Ukubwa wa vitanda hivi ni 4 by 6, na tumeweka godoro la 4 by 6 inch 8....(hatutoa karatasi za godoro maana bado kuna kazi zinaendelea......yasichafuke) na godoro waweza kuweka lolote lile kulingana na uwezo wako na kukapendeza.
Karibuni sana mtoe orders......

Tuesday, May 1, 2012

Nimewagusaaa eheheee!!!!






Inafika pahala sasa tuambizane ukweli....., watanzania asilimia kubwa hatuna hela si ndio ehee, ila hao hao utawakuta wanavaa vizuri, tena vitu vya designers, kama ndio nguo, cheni, viatu (CL) ndio vimeingia maana navisikia tuuu, lace wig kuchangia sherehe kwa kiasi kikubwaa cha fedha etc.

Wanakokaa hapafai na ni aibu jamani, yaani unamkuta mtu nje mrembo kavalia huyoooo, gari zuri ila nenda home kwake, jamani, unaweza ukakataa lol...

Hivi kweli uki save hela yako hiyo ukasema sasa mwezi huu ama miezi miwili sinunui nguo wala viatu etc, natengeneza nyumba yangu, kama ni yakupanga ama ya kwako, utashindwaaaa kweli, ama ndio kupanga kuchagua....

Hebu tujirekebishe sasa, na tuanze kupenda nyumba zetu, maana maisha yetu yanategemea sana nyumba zetu, na ukiipendezesha nyumba yako, basi na hata safari usizozipangilia na mafoleni haya kumaliza mafuta ya gari, na uchovu hata kama unapanda basi, zitapungua na utakua unarudi home kwako moja kwa moja kwa amani, na utapumzika kwa amani.....


Ni hayo tuuu kwa leo.........TUBADILIKE, NA HILI LINAANZA NA WEWE, SIE WENGINE NI WATAZAMAJI TUUUUU UKIJIBANA KWA MUDA UNAWEZA KUPAMBA NYUMBA YAKO NA IKAWA NZURI TENA ZAIDI YA HIZI............



1 Room, 2 looks






Picha zinajieleza jamani ama sio...........

Sunday, April 29, 2012

Surprise..........

Habari za weekend, yangu ilikua poa, ila na hii mvua......iliniishia nikiwa site za wateja... si mnajua kazi tena hua sina weekend mara nyingi ninakua site...


Nina surprise kwa ajili yenu, unapenda kuijua ni nini?


Endelea kupitia blog hii yetu ndani ya wiki hii ya mwanzo wa mwezi huu wa tano......


Love u all..... Nawatakia wiki njema na mei mosi njema....


Sy

Friday, April 27, 2012

SOLD


Mnaikumbuka hii set, ina 3 sitter 1, 2 sitter 1 na single sitter 1....
Shelf pekee ndio inauzwa...waweza weka vitabu, urembo etc...
Meza ya viti 6


Sofa wanakaa watu 6. 3 sitter, 2 sitter, na 1 sitter.

viko katika hali nzuri... na vina umri mdogo sana... tuwasiliane kwa atakae hitaji.... 0713 - 920565...Karibuni

NB:
Nimeanzisha kipengele hiki, kwa atakae hitaji kuuza furniture zake, tuwasiliane na nitaviweka kwenye blog kwa mauzo.....ila viwe na hali nzuri, na nitakuja kuvikagua kwanza kabla sijaviweka humu...kwa watu wa mikoani naomba mvipige picha kila kona ili niweze kukagua......

Tiles.........(Nilitembelea CTM Mwenge wana tiles nzuri, na nilipata maelezo ya kutosha na kuwaletea makala hii).....




Nikiandika maelezo kutoka kwao...
Ni baadhi ya mabafu ya kisasa waliyonayo...
Mabomba ya kisasa waliyonayo.....kwa kweli ni mazuri sana...



Display ya mabafu waliyonayo..... hivyo unachagua upendayo....(jamani jamani, bafuni, na jikoni, sio sehemu yakuweka tiles zinazoteleza... maana wengine wanadondoka wanasema ni nguvu za giza, ama visingizio kibao, kumbe ni tiles ulizoweka zinateleza....sasa ukienda kwa mawakala watakushauri, na utanunua vitu quality)




Display za tiles zimepangwa kwa square metre kabisaa... na wana designs nyingi. nimewapenda sana kwa kutoa ushauri, na bidhaa zao ni quality.....
Katikati ya wiki hii, nilipita CTM pale mwenge kituo cha ITV, hii ni kampuni ya tiles, sanitary ware, (masink, mabafu ya vyooni etc)& brass ware (mabomba).

Niliongea na mwakilishi wa kampuni hiyo, kwa kutaka kujua matumizi ya tiles, na wapi tunaweka, kwa sababu nimeona kuna matatizo ya uchaguzi wa tiles.....

Types of Tiles;
Tiles za ukutani (Wall Tile)
Tiles za sakafuni (Floor Tile)

Designs of tiles:
Ceramic - hizi zina urembo
Porcelain - hizi ni za kung'aa, sasa hapa kuna zinazoteleza na hazitelezi.
Corto ama outdoor - hizi ni za nje, hata ndani waweza weka ila jikoni.
Kilimanjaro tile- zinatengenezwa south africa, kuna za ndani na za nje na hazitelezi.

Sasa kabla ya kwenda kununua tiles haya yafuatayo ni lazima uyajue.

Ujue unataka kuweka wapi,
matumizi ya hicho chumba,
na vipimo hua vinahitajika kwa square metre.

kampuni hii malighafi zao zinatoka:
South Africa
Brazil
Spain
China.

Umuhimu wa kununua tiles kwa mawakala ni kwamba, huwezi kupata vitu feki, wa ujanja ujanja.... na vinakua na guarantee....

Kwa mawasiliano zaidi, wanapatikana hapo mwenge kituo cha ITV, wako barabarani kabisa.....Karibuni

NB:
nitakua nikiwaletea makampuni yayouza vitu orignal, na ni mawakala na vyenye guarantee.... sasa na pia kama unataka kujua kitu chochote kile, niambie na nitawafuatilia na kuwaletea humu...
UMEFIKA MUDA SASA TUACHANE NA VITU FEKI... FEKI NI GHARAMA....(nyumba yako na unakaa mwenyewe, ila bado unachakachua... lol......haipendezi......tuachane na hiyo dhana sasa....)

Nawatakia weekend njema.......