Tuesday, June 18, 2013

Site ya Tabata........

 Katika site hii tulipeleka kitanda cha size 5 by 6, cha chuma....Hapa mafundi wakifunga kitanda...

LEATHER SOFA.. SOLD......

 Sofa sets zinauzwa......ziko seti mbili, nikiwa na maana 3 sitter 2, 2 sitter 2, na 1 single sitter 4... ni pure leather....

PRIMARY COLORS

Niliahidi kutoa somo la rangi wiki zilizopita, ila kwa bahati mbaya tukawa tumepata tatizo la internet.





Sasa basi katika somo la rangi nimeona nianze mwanzo kabisa....ili liweze kutusaidia, na tuweze kujua utumiaji wa rangi, na rangi zipi zitumike wapi na kwa muendelezo upi ili upate mandhari ipi na ulioikusudia.

Primary Colors.....

Primary colors ziko tatu, ambazo ni Nyekundu, Bluu na Njano.  Rangi hizi zimepewa jina hilo kwa sababu zinajitegemea nani rangi za mwanzo kwa upatikanaji wa rangi...haziwezi kutengenezwa kwa kutumia rangi zingine zikatokea hizi primary colors...Nikiwa na maana huwezi kuchanganya rangi flani na flani ukapata njano ama blue ama nyekundu.....

Rangi hizi ndio kianzio cha kupatikana  rangi zingine kwa kuchanganya rangi mbili tofauti katika hili kundi la primary colors. Hua tunaziita pigments.

Mchanganyiko huo wa rangi  mbili ndio unaofanya rangi kuvutia, na kupata rangi uliyoikusudia, ikichanganywa kwa uangalifu na kwa kiasi kinachohitajika.

Kwa mfano kupata rangi za nyumba, za wachoraji etc.....lazima watumie primary colors ili kuweza kupata rangi zingine na ambazo wamezikusudia......

Somo litaendelea........



Tatizo la Internet.....



Homez Deco tunaomba radhi kwa kua kimya, na hii ni kutokana na internet provider wetu kua na matatizo ya kiufundi.

Ila sasa tumerejea tena hewani.

Nawashukuru kwa uvumilivu wenu..

Sylvia Namoyo,
Director.

Wednesday, June 5, 2013

Kifuatacho: Jinsi ya kuchagua rangi za nyumba/office yako.......

Nimepata maombi yenu wadau kua mnaomba niwaelimishe kuhusu kuchagua rangi za ndani, za nje. za nyumba zetu na ofisi zetu......sasa basi nitawaletea somo hili kutokana na maombi mliyoyaomba.......


Tuesday, June 4, 2013

Marble counter tops.......


 Nilitumiwa comment na mmoja wa mdau wetu anaomba kusaidiwa ni product gani nzuri kwa ajili ya kusafisha marble counter tops.....maana zinashika mafuta, na uchafu na kuweka madoa.

Marble hizi zinawekwa jikoni ama bafuni......na katika utunzaji wake na usafishaji wake hazitaki kusuguliwa ama kukwaruzwa......wakati wa kusafisha....na zinahitaji sabuni ambayo haina kemikali katika kusafisha.....
 Marble ziko za aina nyingi na rangi tofauti........


Hii ni product itakayofaa kwa kusafisha marble za aina zote na usafi wowote ule katika nyumba yako ama ofisi.......na hiyo ni chupa yake mahususi maana ina vipimo kulingana na uzito wa uchafu....

Unachotakiwa kuwa nacho ni hii super 10, chupa na kitambaa ama kitaulo kisafi cha kufutia uchafu huo....

Hapa kwenye kitambaa kinatakiwa kiwe kisafi...maana kikiwa kichafu hautakua umefanya kitu....

Kwa mahitaji ya super 10 na chupa yake wasiliana na Tija : 0713 - 336977 na atakupa maelezo zaidi ya jinsi ya kuitumia...na demonstration pia atakufanyia......

Metal Furniture........Living room & Dinning....

 Hapa ni living room kukiwa tayari tumeshaweka makochi ya chuma kama inavyoonekana......kwa upande wa rangi ya nyumba, tayari ilishapakwa na wenyewe. sasa homez deco ilihusika na makochi, coffee table na dinning table......nyumba hii imepakwa rangi ya papaya na purple.....
 Hii ndio dinning table ya watu 6
 Niliwashauri waweke picha za ukutani...na wakakubali....hivyo wakiwa tayari nitawashauri jinsi ya kuweka.....kwenye swala la picha bado tuko nyuma....tunatundika picha juu sana ama chini sana....na hazilingai...picha zinatakiwa ziwe eye level...yaani usiinue macho kutazama picha.....



 Hapa ndio tulikua tukiingiza furniture ndani......
 Furniture za chuma hupendeza kwa kweli...na hufanya nyumba kua safi wakati wote...maana unaona mpaka chini ya uvungu kama ni kuchafu ama kusafi.....
 Nikiwa nimekaa kwenye kazi yangu......

Nawashukuru wateja wangu kwa kuridhika na kazi yangu......nawatakia kila la kheri......