Monday, November 11, 2013

KWA WALE WOTE WENYE WATOTO WATUNDU WANAOCHORA MAKOCHI........RANGI ZINAZOFAA ZA MAKOCHI.....

 Habari za muda kidogo wadau wangu, nilikua kimya kutokana na majukumu ya kifamilia kidogo, na sasa tuko sawa.

Sawa, sasa kuna tatizo kidogo, kwenye uchaguzi wa makochi ya kwenye nyumba zetu, kwa wenye familia ya watoto wadogo, kwanza kabisa ninachoweza kusema ni kua mtoto ukimfundisha anaelewa, na ukimdekeza atakupa hasara..........sasa ni wewe tuu uamuzi wako.......

Nimekutana na tatizo hili la makochi kuchorwa chorwa na watoto wetu, na jamani bei za makochi tunazijua zilivyo gharama........na pia kwa kua tuna watoto basi hatuna budi kununua makochi ambayo rangi zake ni dark na sio light.......kupunguza tatizo la watoto wetu kuchora kwenye makochi yetu.....

Hebu fikiria umenunua kochi lako kama ndio off white ama cream then likachorwa chorwa na mtoto, kama ni cartoons ama ndio anajifunzia homework etc......


 Nimejaribu kuleta baadhi ya rangi hapa ambazo hazitaonyesha uchafu wa kuchora wa watoto wetu.......
na kwenye accessories ndio unaweza kuweka rangi ambazo ziko light maana itakua rahisi kuzi maintane na kusafisha ama kufua......

 Ninaomba kuwasisitiza wadau kuwafundisha watoto wetu kua hawatakiwi kuchora kwenye makochi, ama ukutani.......na hili linawezekana kabisa...watoto wanaelewa ukiwafundisha.......(mbona shuleni wanaelewa na wanafaulu....sasa itakua nyumbani kuwaelekeza kua wasichore makochi na ukuta etc)

3 comments:

  1. eeh! hatimae umerudi blog itakuwa active tena, wellcome back!!! sasa naomba unisaidie jinsi ya kuosha madumu( vyombo) vya kuhifazia maji, nimetumia njia mbali mbali but naona bado ile rangi ya kijani imekataa kutoka, yanaoneka machafu kweli coz ni meupe na mkono haupenyi ndani..
    thanx, mdau wa Arusha.

    ReplyDelete
  2. kuosha madumu yenye rangi kijani ndani tumia jiki, water guard au chlorine powder loweka kama saa 12 halafu osha kwa sabuni ya unga.

    Mdau: Kigali, Rwanda

    ReplyDelete
  3. Je mna care products kwa ajili ya leather sofa km cleaner spraz, protector na conditioner, km ndiyo zipatikana kwa bei gani

    ReplyDelete