Monday, December 3, 2012

Maandalizi ya X-mass kwa upande wa vyombo.....

Nadhani tunakubaliana kua, bado kuna watu hua wanaweka vyombo makabatini, havitumiki mpaka mgeni aje ama siku za sikukuuu....sasa basi hiki ndicho kipindi cha maandalizi ya vyombo hivyo...

Vyombo hivi hua vimekaa muda mrefu sana kabatini......inabidi kuanza kuviandaa kwa kuviosha vizuri, maana uvundo wake kuondoka hua unachukua muda, nikiwa na maana harufu.....

Kwa msaada, nashauri utumie sabuni ya LDC ya GNLD, ni nzuri na hukata haruhu hizo, na hung'arisha vyombo vyako na matumizi yake ni kidogo mno......

Hii ndio sabuni ya LDC......ni 1Litre....matumizi yake ni kidogo mno, ukilinganisha na sabuni zingine...Bei ni 26,000/-

Baadhi ya vyombo vikiwa vimeandaliwa mezani......








Hizi ni baadhi ya set up za  meza kwa ajili ya x-mass.........haijalishi una vyombo vya aina gani, meza ya aina gani....hiyo hiyo uliyonayo...inafaa kwa set up...ni kuiandaa vizuri na itapendeza......

No comments:

Post a Comment