Hizo pictures ni baadhi ya maeneo ambayo tumefanya kazi za gardening kama mnavyoona, mbolea ni muhimu sana, udongo unaostahili maji, yawe ya kumwagilia yawe ya mvua ni muhimu, hapo tulikuwa tunaweka mbolea kwenye miti maua, sehemu mbalimbali za gardens, si kwamba ukiishapanda miti basi umemaliza kuna kuongeza mbolea majani, plunings kuna vitu vingi sana vinavyoitajika ktk kuboresha gardens,zikaonekana nzuri na za kuvutia,
Huku new york tunatumia mbolea aina ya mulch, na hizi mulch kuna za ina tofauti kuna red mulch kuna black mulch kama mnavyoona hapo kwenye picha.
kwetu sisi black mulch ni nzuri, ina ubora zaidi na mimea yawe maua iwe miti bushes vinastawi sana, jambo lingine wapendwa ni vifaa ktk hii kazi ya landscaping vifaa vya kufanyia kazi ni muhimu sana vinarahisisha kazi, unaokoa muda, na nguvu, maana mfano mzuri ni Dar watu wa gardens wanachukuwa mrefu kumaliza kazi,, kwa kuwa wengi wao hawana vifaa ya proper gardening tools, ila ninawapongeza sana wanafanya kazi kupendezesha jiji,
majumbani sehemu za bihashara, nawaomba watanzania wenzangu tuyapende mazingira yetu tunayoishi, pandeni miti, maua unakuta mtu amejenga nyumba nzuri tu ila mazingira ya nje ya nyumba ni yakusikitisha, iweje ugaramikie jumba la garama ushindwe garden nzuri ?
baadhi ya watu wanasubiri mvua zinyeshe wafungulie septic tanks mtaani,malundo ya takataka mbele za nyumba zenu uchafu kila kona , hii ni hatari sana vyanzo vya maambukizi yamagonjwa, chloea, kipindupindu, huu wote ni uchafu uchafu, jitaidini wapendwa kuwa wasafi kuyasafisha mazingira mnayoishi,usafi ni muhimu sana ktk afya zetu, majumbani, kwenye mikusanyiko ya watu, , kwenye migahawa, shm za kazi
haya yote ynaanzia ngazi ya familia, mpaka taifa jitaidi wapendwa, nasisitiza usafi kiujumla, wa mazingira, mnayoishi ziwe nyumba za kupanga au yakwako binafsi usafi ni wajibu na muhimu sana yalinde yatunze mazingira yaliyokuzunguka daima,
mungu awabariki na kuwalinda
No comments:
Post a Comment