Thursday, June 7, 2012
Remba nyumba yako kama designer.......(tembelea website yetu www.homezdeco.co.tz)
Nime kua kimya kidogo, ila nashukuru mungu kila kitu kinaenda vizuri, kuna projects mbili tatu hivi nakimbizana nazo. ila sijawasahau kabisa wadau wangu.......
Kama nilivyowambia mwanzoni mwa mwaka huu kua nitakua ninatoa somo la decor kwa kiundani kiasi na nitapunguza kwa kiasi kikukubwa ku download kazi za wenzangu, sasa kama kuna mtu ninamuacha aniulize ili twende sawa. si unajua mtu akikaa kimya jua kua kaelewa... hhhahha
Leo nitaongelea kitu kinaitwa Mood Board......
Mood board inatumiwa sana sana na designers, wawe wa nguo, wa majumbani etc, wote twatumia hii....
Mood board ni kifaa kinachotumika na designers kuweza kuwasaidia kupata mawazo ya wateja wao wanahitaji nini.
Mood board hua ni mkusanyiko wa picha za magezitini, michoro, vitambaa, rangi, etc.
Sasa basi ni jinsi gani unaweza kutengeneza Mood board yako na ikawa ni nzuri na ikakusaidia kuremba nyumba yako?
Angalia magazeti ya home decor, ama picha, etc, na utakapoona na ukapata rangi unazozitaka, basi kata kipande cha hiyo picha na viweke pembeni, tafuta pia sample za vitambaa, vya mapazia, ama vya sofa na uviweke pembeni, carpets pia picha zake, na kila kitu unachokiona kua unakihitaji nyumbani kwako...... ukiwa umekamilisha hili..
Tafuta kipande kigumu cha kiubao na ugandishe hizo picha zako, na ukiona umeridhika na hayo matokeo, basi ujue kazi iliyobaki ni utendaji....
Hii husaidia sana sana kukurahisishia usichanganye rangi zisizoendana, na kadhali, yaani itakulinda pia kwa upande wa budget......
Mahitaji:
Magazeti ya home decor
mkasi
ubao
pen
pesil
gundi
rula
na hapo sasa unaweza kuwa tayari kwa kuanza kazi yako,
Waweza pia kutengeneza mood board yako kwa kutumia computer, ukiona unachokipenda copy, save kwenye folder moja, na uje uziunganishe...
Hapo juu nimeweka baadhi ya mifano ya mood board....itakayokusaidia kupata aidia ya nini unatakiwa kufanya na itaonekanaje.....
NB:
Elimu ninayotoa kwenye wadau, sio lazima niifanye mimi, waweza ifanya wewe na nikakusaidia, kwa ushauri ama utakapo kwama, ama hata ukipata mtu akakufanyia, basi angalau nawe unajua ni nini kifanyike, ili uweze kumsahihisha na ukapata kile unachokitaka, kwa watu wa mikoani sana sana....
Kwa leo ni hayo tuuu....
kwa maswali karibuni.....
Labels:
Advice
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sylvia, wall papers zinapatikana wapi Dar? Sorry ni nje ya topic. Asante
ReplyDeleteHi sylvia, naungana mkono na mwenzangu hapo juu, ningependa kufahamu wapi zinapatikana wall papers hasa za kuweka chumbani kwa mtoto.
ReplyDeleteNakupongeza sana kwa kazi nzuri.