Chumba cha kulia chakula:
Chumba hiki kinahitajika kua na mwangaza wa wastani. Taa za ukutani, taa za picha(urembo) za ukutani na taa za mezani ni chaguo lako. Unaweza ukapata mwanga wa kutosha kuzunguka meza kwa kutumia taa za glopu ndoga ama taa ya kuning'inia ama zote kwa pamoja.
Taa zenye mwanga mdogo huongeza nakshi ya muonekano sehemu ya kulia chakula..
Chumba cha kulala:
Chumba huhitaji mwanga mdogo muda mwingi, japo kua mpangilio mzuri wa taa unahitajika ili kupata mwanga unaohitajika kwa ajili ya usafi na kufanya shughuli zingine kama kukunja nguo, kupaki vitu, kuvaa etc. Hii inaweza kutolewa/kuwezeshwa kwa kuchanganywa kwa taa za ukutani, taa za juu ambazo zinaweza kua na mwanga hafifu (zinazopunguzika na kuongezeka mwanga) hua na muonekano wa kuvutia.
Mwanga mzuri wa taa za pembeni ya vitanda (bedside lamp/lights) ni mfano mzuri. Hii inamaanisha, weka taa ambazo ni maalum kwa kusomea(reading lights/bedside lamps). waweza weka taa zenye urembo, rahisi kutumia, na zinazodumu na zenye kuvutia.
NB: Naomba ieleweke kua kabla ya kununua taa jitahidi sana ujue ina mwaga wa kiasi gani, na kama ina matumizi gani,... maana unaweza nunua taa ilimradi taa tuuu, kumbuka kuna vyumba havi hitaji mwanga sana, na kuna vingine vinahitaji mwanga, sehemu kama jikoni, mwanga ni lazima wa kutosha, kwenye vyumba vya watoto kuchezea, nje etc.... ila kwa mahali kama chumbani mwanga mwingi hauhitajiki... maana hapa ni sehemu ya kupumzikia so hakuhitaji sana mwanga, na ninashauri chukua taa ambazo zinapunguzika mwanga kama nilivyoongea hapo juu. hebu fikiria umerudi umechoka kazini,halafu unaingia chumbani unawasaha taa, mwanga huooooo, si utaumwa na kichwa wewe jamani? ............
Topic to be continue...... Bathroom lights, Playroom, and Utility room.........
No comments:
Post a Comment