Nategemea bado mnaendelea kuyapenda mazingira na kuyarinda maana tusipo yalinda mazingira tunayoishi na kuwa wasafi tutakumbana na milipuko ya magonjwa, mbalimbali, nawasisitizie kuanzia ngazi za familia usafi wa nyumba zetu, migahawa na sehemu zote wanazotoa huduma ya vyakula tuzingaie usafi tunawe mikono kila mara, tuwafundishe watoto wetu, Pia tuepukuke uchafu marundo ya takatka mitaani kwetu, kwenye mitaro vituo vya mabasi hivi vyote ni hatari sana kwa afya zetu, tuwe makini sana sehemu za bihashara za vyakula vikavu vibichi,
pia jamani watu wenye mabucha jamani inatia kinyaa unapoingia buchaa mainzi warukaruka kila sehemu kwanini hamuweki milango ya nyavu??? na kuifadhi nyama ktk majokofu wapendwe? pia baadhi ya masoko mvua zikinyesha ni balaa ni uchafu matope yaani ili jambo linanikeraga sana hasa masokoni yaani hakuna anayeliona hili jambo au ndio tunasubiri ziundwe tume, nyinyi wafanya bihashara mnashindwa kuwa na utaratibu mzuri wa usafi , sehemu ambayo imekidhiri na uchafu ktk masoko ni kwenye machinjio ya kuku yaani uchafu uliokidhiri hata hamu kununua kuku inakuishia, sidhani ni mimi tu maana kila leo wateja mnaenda na kupata mahitaji yenu ili mmlifumbia macho suala la usalama wa afya zenu, huko hatarini sana .
Mi nasisitiza uasfi kwenye sehemu zote, zinazotuzngka kimazingira, iwe ni kibiha shara, majumbani, kwenye restaurants , saloons mahospitalini kwenye majengo ya serikali na kwingineko usafi uimalishwe, si kwenye mavazi tuu ni idara zote ttulipende jiji letu usitupe taka hovyo, abiria urushe machupa barabarani, mifuko ya plastics, mabaki ya vyakula, wapendwa tulimishana. linda mazingira nayo yatakulinda.
watanzania wenzangu tuipendezeshe nchi yetu. From Jossyane G -
No comments:
Post a Comment