Monday, November 8, 2010

TUJALI MAZINGIRA TUNAYOISHI NYUMBA ZETU, MAKAZI YETU IWE OFSINI

Leo nazungumzia mazingira kwa ujumla majumbani mwetu, sehemu za biashara maofsini wapende sehemu hizo zinaitaji usafi na si ubabahishaji,

unakuta  migahawa baadhi ya nyumba zina vyoo vichafu vichafu hii hi hatari sana kwa magonjwa ya kuambukiza kipundupindu ndugu zangu kipindupindu ni uchafu uliopitiliza, kutonawa mikono kila mara tunapotoka msalani, pia nakutozingatia usafi wa hizo sehemu mara nyingi sana baadhi ya  vyoo na mabafu, ziwe vya kulipia au majumbani ni vyanzo vikubwa vya magonjwa ya milipuko mojawapo kipindupindu, wafundisheni watoto wenu iwe ni mashuleni waalimu lazima muwafundishe watoto umuhimu wa usafi wa vyoo mabafu ni muhimu sana. na usafi wa kila sehemu kwa ujumla 

  iwe jikono, sebuleni nje ya nyumba, Na kunawa mikono kila mara maana virus zinasaamba kwa njia ya kushika vitu kupeana mikono kukohoa,lazima 

  usafi upewe kipaumbele kikubwa ktk jamii, wafundisheni watoto ukikohoa lazima uweke uzibe kinywa chako kwa kitambaa kisafi cha mkononi , ukitema makohozi yafunike, na tabia nyingine inayonikera ni kuingiza vidole puani ni uchafu uchafu unakuta mtu anauza chakula , matunda anaguna pua na vidole ni uchafu uchafu tumieni handchiefs au kitambaa cha mkononi jamani, nimeona hii mara nyingi hata kwa watu wazima acheni ni aibu sana hili jambo pia ni njia mojawapo ya kuambukizana magonjwa kama mtu ana TB,

tuwe wangalifu sana. na kuwa wasafi ktk nyumba zetu na sehemu zote kwa ujumla ila tuzipende nyumba zetu nyumba zetu kwa wakina mama wote wakina dada hata wakina baba siku zote nyumba yenye choo au bafu chafu basi jua kabisa jikoni ni jalala,

Ndio maana tunawataalum kama dada sylvia atakusadia kukupa mwanga na mpangilio mzima wa nyumbani kwako au ofisini kwako kuweka mapazia kupamba maua , au kupiga rangi ni rangi gani upige maaana wengine mna rangi za kuumiza macho rangi  zenye giza kwenye nyumba jamani DAR rangi zinazoitajika ni light colors siyo dark colors maana DAR N muda wote, una hitaji msaada muone slyvia atakushauri ni nini cha kufanya, 

No comments:

Post a Comment