Thursday, August 20, 2009

Usafi wa jikoni

Habari za leo ndugu zangu.  Leo nimeguswa sana na upande wa usafi wa jikoni. Jamani utakuta jikoni kwa mtu dasta analoshikia sufuria halitamaniki lol! Chafu kupita kiasi, vitu kama madasta, ya jikoni yanatakiwa kuwa masafi masaa yote.

Kuna aina za madasta ya jikoni:

  • Dasta ya kushikia sufuria wakati iko jikoni na kuepulia
  • Dasta ya kufutia meza za jiko
  • Dasta ya vumbi
  • Dasta ya kufutia vyombo(hapa sasa zimegawanyika, kuna ya kufutia glass, na ya vyombo vingine na ya masufuria. na inatakiwa isiwe ya matirio ya nailon, iwe cotton ndio itafyonza maji vizuri) Ukimaliza kazi na hizi dasta fua na uziloweke.

Mavazi pia sijasahau kuna vitambaa vya kuvaa vyaitwa appron, hivi huzuia nguo zako kuchafuka wakati ukiandaa chakula(haijalishi kama unajiko ndani ama nje).

Kwa upande wa makosheo ya vyombo, pindi umalizapo kuoshea vyombo, suuza na weka sehemu safi, kama unatumia sabuni ya kipande basi iweke ndani ya kikopo na uwe umekitoboa kwa chini ili kiruhusu maji kuchuja ili sabuni iwe kavu muda wote.

Mimi binafsi huwa sipendi kuwa ninapika na huku vyombo vimenijalia kibao kwenye sinki, ninatayarisha kwanza vitu vya kupika na nikianza kupika huku navikosha vyombo nilivyotumia, huku ni kusevu muda kwani unapokuwa unapika na kuosha vyombo unaweka jiko lako kwa hali ya usafi muda wote. Kama maji hayatoki kwako basi vihifadhi kwenye beseni vizuri kisha vifunike kwa hali ya usafi ukimaliza pika osha.

Namshukuru sana mama kwa malezi bora bila kusahau na elimu pia. Mama asante sana(NAKUPENDA SANAAAAA)

Ila jamani tuseme tu ule ukweli usafi ni wewe mwenyewe ulivyojiamualia. Ukitaka kuwa msafi utakuwa ukitaka kuwa mchafu utakuwa tuuu ama sivyo?

No comments:

Post a Comment