Wednesday, July 31, 2013

Moses busket Inauzwa.......


Imetumika miezi 2 tuuuuu bei ni 300,000/-

Wasiliana na 0657-417070 Sylvia. (ni wajina wangu)....

Ukarabati wa vyumba vyetu katika kipindi hiki cha kuelekea kusherehekea sikukuu.............

Tumeshazungumzia, sebule, dinning, korido, vyooni na sasa tunaelekea vyumbani na kisha tutakuja jikoni, na nje ya nyumba zetu.......

Katika eneo hili la chumbani, hapa ni mahali pa kupumzika, ama kulala unapohitaji, kama ni usiku ama mchana.......Mwili unahitaji kupumzika, na kama unahitaji kupumzika, basi hakuna budi chumba kiwe kisafi, kizuri, na kiwe na nafasi....

Hivi mi jamani hua ninashangaa kwakweli, kuona vyumba vimejaa vitu. na kama mnavyojua vyumba vyetu vya kulala hua ni standard size....kama ndio 12 by 12 ama 10 by 10....kama ni nyumba ya kupanga ama ni nyumba yako.......sasa kwanini mtu usiweke vitu ambavyo utavitumia, na kuliko kurundika vitu?

Kwa mfano, unakuta mtu kaweka kitanda 6 by 6, makabati , dressing table, shoe rack, stand ya pochi, na tv, kochi, hanger ya nguo etc......basi ni kurundika vitu tuuu

Cha msingi jamani kwanza angalia ukubwa wa chumba chako, na ikiwezekana ukipime kama hujui size yake....na baada ya hapo, weka vitu kulingana na ukubwa wa chumba......sasa utakuta chumba ni kidogo lakini mtu anaweka kitanda kikubwa ama kabati kubwa.....yote haya ni ya nini?

Na huko kwenye makabati kuna nguo nyingi mtu na zingine hazivaliki......yaani kabati mpaka linalemewa....sasa ukija kwenye viatu ni vingi mno, na vingine huvai labda kwa kuharibika, ama umevichoka....ila bado unavyo tuuuuu....

Naomba kushauri kua vitu ambavyo hutumii jamani GAWA......

Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata nafasi na hewa izunguke katika chumba chako, kua na vitu vingi sio kupendezesha nyumba........

Kwani ukiweka vitu kulingana na chumba chako, tena kwa mpangilio kutakua na tatizo?

Kwa upande wa rangi za vyumbani, tafadhali rangi zipakwe zilizopoa, maana rangi nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa mno katika kukufanya u relax.....

katika vyumba vyetu tukumbuke pia usafi wa kina, ukianzia usafi wa cyling board, madisha, mashuka...etc.....

Dressing table zetu jamani hua tunazisahau.......mafuta yakidondokea hua yanaacha alama, vitana navyo....etc

Rangi hizo baadhi ni.................
 Kama rangi ina kiza, basi ipakwe kwenye upande mmoja wa ukuta na  kuta zingine ziwe na rangi ambazo ziko angaavu...

Thursday, July 18, 2013

Public Toilets and Bathrooms....

Umeshawahi kukutana na toilet ambapo ukipita kwenye korido, unasikia harufu mbaya inatoka na kusambaa korido nzima, ama kama tena na hiyo toilet iko karibu na sitting room ama dining room basi ndio harufu yote inasambaa................

Kumekua na tabia kwa asilimia kubwa, watu kudharau ama kuona kinyaa kufanya usafi kwenye vyoo....vya nyumba zao...ama kumuachia tuu msichana wa kazi afanye usafi ajuavyo bila kumfuatilia usafi umefanyika vizuri tena kwa dawa zinazotakiwa kutumika, maana utakuta ukuta una ukungu ama kutu , masinki nayo basi vurugu tuuuuuu.......

Tuesday, July 16, 2013

KORIDO ZA NYUMBA ZETU....


Naomba leo tuangalie upande wa korido, baada ya kua tumeshaona sitting room, dinning room........

Katika eneo hili, kwa upande wa kuanzia usafi na rangi ni muhimu sana kuzingatia
Korido nyingi hua hakuna dirisha ama madirisha...hivyo kunakua na kiza cha aina flan hivi.......kulingana na ulivyojenga.

Hapa kuna nyumba aina mbili: kuna ambazo ni fupi na kuna ambazo ni ndefu (urefu kutoka juu mpaka chini).......ingawa wengi wetu tunajitahidi kujenga nyumba ndefu kulingana na maendeleo na mabadiliko ya kila kukicha.

Mtakubaliana nami kua kwenye korido zetu hua zinachafuka mno, maana utakuta mtu akipita mwingine kashika na mikono yake michafu, ama mwengine anashika tuuu basi ilimradi tabu tupu, na hivyo kufanya korido kuchafuka, na kama ndio haukua umepaka hizi rangi za wash 'n' ware ama silk maana rangi za aina hizi hua unaweza kusafisha na maji na uchafu ukapungua ama kuisha kulingana na uchafu wenyewe.

Kama unaona ukuta wako hauridhishi, basi waweza kupaka rangi, kwa kuuandaa ukuta wako. Mwite mtaalam, akupe hesabu ya rangi inaingia kiasi gani na gharama zake na aina ya rangi.......hivyo atauandaa ukuta kwa kupiga msasa, na kuziba mashimo kama yako, nashauri mtumie skimming plaster smoothover za dulux, halafu apake rangi iliyokusudiwa kama ni za Dulux etc.......

Rangi za korido ni light colors, ama rangi zenye mwangaza......Kumbuka katika eneo hili hakuna madirisha hivyo mwanga kupenya ni asilimia ndogo mno, ni nyumba chache zenye madirisha katika eneo hili.

Sasa unapopaka rangi zenye kiza, korido inakua ni ndogo, na giza na haitakua na mvuto wowote, hata kama kuna taa ambazo utaziwasha wakati wa usiku.......

Baadhi ya rangi za kupaka korido ni hizi, ingawa inategemea pia na sitting room na dinning room umepaka rangi gani......

Dawa Ya Mende....

hongera sana kwa kazi nzuri unayofanya. nina shida moja nahitaji msaada wako nyumbani kwangu kuna mende sana kila sehemu , kama unaweza kujua dawa nisaidie hili nilitatue hili tatizo.  nijibu kupitia blog yako.

asante sana
mimi-Anna 


Homez Deco tumepata email hii kutoka kwa mdau wangu na anaomba usahuri kama inavyosomeka.....Na napenda kumjibu hivi.....

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta sababu ya mende kuwa katika nyumba yako, na sababu ni kati ya hizi, :
1. hauweki vitu kwa mpangilio
2. nguo ni nyingi na ziko katika malundo
3. hautumii products nzuri za usafi
4. uchafu uliokithiri
5. mabaki ya chakula hayatupwi sehemu husika na kwa usafi
6. usafi pia haufanyiki ipasavyo etc...
Hizi ni baadhi ya points ambazo ningependa uzifanyie kazi.....kuanzia nje mpaka ndani....na inahitajika uache kazi ufanye kazi, nikiwa nina maana kua ujitolee siku moja ufanye usafi wa nyumba nzima.......ikiwezekana utoe vitu nje vipigwe na jua kwa muda hata wa siku mbili ama tatu, na ndani ufanye fammigation pamoja na nje.....
Kabla ya kuingiza vitu ndani, hakikisha unachagua vitu unavyovihitaji, usivyo hitaji kama viko katika hali nzuri gawa, kama havifai basi tupa sehemu husika.......

This time ingiza ndani vitu utakavyotumia na upunguze mlundikano wa vitu.....na usafi uwe ni wa mara kwa mara, na kwasababu umefanya fammigation, ile ni sumu fanya usafi vizuri........

NB:
Hakikisha unahusisha na majirani katika fammigation maana ukifanya wewe mende watakimbilia kwa wenzio. dawa ikiisha nguvu mende wanarudi.......

Homez Deco tunakaribisha ushauri zaidi.....


Friday, July 12, 2013

UPAMBAJI WA ENEO LA KULA CHAKULA ( DINING AREA)

Leo tuingie upande wa dining area, katika chumba hiki wengi wetu katika nyumba hua kinaangaliana na sitting room, na kwa wachache hua wamekitenga yaani kinakua na ukuta hukioni.....

Tuanze na kwa hawa ambao dining inaonekana......katika ukipamba chumba hiki, angalia kwanza unahitaji kiweje yaani kiwe na mandhali gani, na kisha angalia ni nini na nini ni cha kuondoa. kama kimechakaa ama kimekwisha, ondoa ili uweze kupata nafasi nzuri kwa kuweza kudesign.

Kwa wale wenye dining room inayojitegemea unaweza paka rangi tofauti maana humu kunajitegemea......

Ingia mitandaoni, ama nunua magazines za home deco...angalia mipangilio iliyoko huko na mpaka rangi.....halafu ukisha jua ni nini unataka, viandike, na uanze kutafuta, sasa hapa waweza kuja kwa mtaalamu wa mambo ya decorations (Homez Deco) ama ukafanya mwenyewe.

Fanya window shopping kwanza, na uangalie pia na ukubwa wa dining area yako.....wengi wetu tuna eneo dogo lakini bila kujua ama wengine hawajali, wanaweka meza kubwa ya watu 6 wakati eneo ni lakuweka meza ya watu 4.....hili jamani tuwe makini katika hili....(Kufanya window shopping inakusaidia kufanya manunuzi ndani ya budget uliyopangilia)

Thursday, July 11, 2013

MITO YA SOFA ........


 karibuni, mito bado iko.................