Tuesday, January 15, 2013
Simple bathroom
Hili bafu ni dogo, lakini jinsi lilivyo pangwa kwa mpangilio....linapendeza.....Ninachoweza kusema ni kua, kwa wewe ulie na sehemu ndogo, nikiwa na maana bafu ni dogo, usilidharau. Liweke katika mpangilio mzuri na usijaze mavitu, ukifikiri kua ndio kulipamba ama kuliweka vizuri.
Labels:
Interior
Monday, January 14, 2013
Color of the year 2013- Emerald Green
Hizi ni baadhi ya design kwa kutumia rangi ya mwaka 2013.....rangi hii inaweza kutumika chumba chochote kile, na unaweza pia ukaipunguza makali, nikiwa na maana ya kua unaweza kutumia dark color ama light color, kwenye ukuta, sofa, carpet, decorations etc....
Labels:
Colour
Inawezekana kwa hapa kwetu Tanzania kua na mzingira mazuri......
Picha zote hapo juu ni baadhi ya sehemu mji wa Florida USA, shukrani kwa MRS. Jossyanne George- Proffessional Landscaper
Mimi binafsi napenda kujifunza kila niwezavyo mbinu mbali mbali,za kupanda miti, maua majani watanzania wenzangu tuyapende mazingira tunayoishi , siyo unaishi kwenye malundo ya uchafu mtaa mchafu ukiuliza siyo nyumba yangu ila wewe ndio unayevuta hewa chafu, magonjwa yakija yanakushambulia wewe na wanaokuzunguka. hasara ni ya nani wewe mpangaji au mwenye nyumba.
Labels:
Gardening
Thursday, January 10, 2013
Chumba kimoja muonekano tofauti....
Hili ni jiko kama linavyoonekana, limebadilishwa rangi mara 5, nani jiko hilo hilo moja. Hivi unajisikiaje unavyokua na ratiba ya kubadilisha muonekano wa nyumba yako ama chumba chako mara kwa mara kadri ya uwezo wako. nikisema hivi nina maana ya kua unaweza ukawa unapaka rangi mara 2 ama 3 kwa mwaka, ama kubadilisha furnitures, kubadilisha mpangilio etc....
Mabadiliko yaanza na wewe mwenyewe, na ndio wengine tunakua wafuasi....
Karibu sana k
Labels:
Interior
Wednesday, January 9, 2013
Ofisi za majumbani...
Nimekua kimya kiasi, ila ni kutokana kuna habari nzuri nitawaambia humu humu.....hivi karibuni, maana haukua ukimya wa bure....
Haya turudi kwenye mada.....Siku hizi katika nyumba nyingi ambazo ninazifanyia kazi asilimia kubwa ya nyumba hizi kuna chumba wamekitenga kwa ajili ya ofisi......na ukubwa wa vyumba hivi vinatofautiana, hivyo nimeonelea nilete angalau design mbili tatu watu waweze kujua ni nini uweke, ama nini ufanye ama kama ulikua hauna lengo la kuweka basi upate hata wazo....
Ofisi za majumbani, hazihitaji vitu vingi, ama marembo mengi....jitahidi ziwe simple na ya kuvutia, na pamba ofisi yako kulingana na ukubwa wa chumba chenyewe....
Weka fanicha za kutoshea chumba, na hakikisha kuwe na nafasi ya kutosha umeiacha, na mwanga na hewa uwe unaingia wa kutosha, kuepuka uvundo.....
Rangi pia ziwe ni angavu na za kuvutia.....kwenye chumba hiki tusipende kuweka rangi za kiza...maana kutakua kuna kusoma, kuandika etc......rangi ang'aavu zitakusaidia kuona na kufanya kazi zako vizuri......
Taa pia iwe ya kutosha kuongeza mwanga....
Labels:
Interior
Wednesday, January 2, 2013
Used Deep Freezer...SOLD
Size: 8 x 3 feet
Height: 2 feet
Volume: 900 litres
Compressor: Danfos
Suitable for: Bar, Supermarkets, Butcher, Shops etc....
Contact 0714 - 222539
Labels:
For Sale
Subscribe to:
Posts (Atom)





















.jpg)
