Thursday, December 3, 2009

Muendelezo wa kazi za mtanzania mwenzetu Mrs. Jossyanne na mumewe hapa kwetu Tanzania

Sio tuu kwamba anafanya kazi huko kwa wenzetu marekani bali hata hapa kwetu tanzania ameshafanya kazi kule lushoto kwa masister. Hii ndio kazi yake aliyoifanya akisaidiwa na mumewe. Dada yetu Jossyanne haogopi kuharibu mikono yake kama wengine tunavyofikiria kuwa eti mara kucha zitaharibika etc.




Wednesday, December 2, 2009

Hii ndio surprise niliyokuwa nikiwatayarishia.

Huyu ni Mrs. Jossyanne George. Ni Mtanzania aishie Marekani, yeye na mumewe wame specialize kwenye Landscaping. Nilifahamiana nae kwa mara ya kwanza alivyoona blogsite yangu mwezi wa nane mwaka huu na ndio ilikuwa bado ngeni, alinipigia simu kutoka marekani na tuliongea sana na kunieleza anachokifanya. Kwa kweli nilifarijika sana na amekuwa kama dada yangu sasa, na bado tunaendelea kuwasiliana vizuri sana. Ninachoweza kusema ni kuwa watanzania tunaweza na tusichague kazi, kama unaiweza na unaipenda ifanye, na Mungu atabariki kazi ya mikono yako. Mimi pamoja na Mrs. Jossyane tutakuwa tukiwaletea makala ya kuwaelimisha kuhusu landscaping walau mara moja kwa wiki kupitia blog hii. nyumbani kwangu (mrs. Jossyanne nikisadiana na mume wangu tumekuwa pia tukipanda maua, miti yaaani shrubs, kwenye majumba ya watu wengine kama hapo picha za hapo chini zinavyoonyesha. Tunaweza kuelimishana, kupitia blog hii, itakuwa vizuri sana, dear, maana, hiii landscaping kwa mfano weather, climate ya dar, na maua yake ni tofauti na ars, au msoma na upandaji wa miti,okay enjoy my dear. Mrs. Jossyanne aliniliuliza kama tunaweza kuelimisha kupitia blog hii nikamwambia inawezekana.


Mr. & Mrs. George

hizo ni baadhi ya kazi zangu tunazozifanya huku new york za land scaping,trimming, weeds killings , morow thae lowans, planting flowers, na mengi tuu. Hii ni kazi yetu sote, mimi na mume wangu tunafanya Land scaping

Mrs.Jossyanne in Thanks giving.

Huyu ndie mumewe wako wote New York City, Mrs. Jossyanne anasema kuwa, huwa wanafanya Thanks giving mara kwa mara na inaweza ikawa ni ya kitu chochote kile, kumshukuru mungu kwa mambo aliyokutendea, kuleta ndugu karibu etc. Mnaonaje na sie tukiwa nayo kwenye familia zetu?
Hapa yuko na shemeji yake na wifi yake

Yami yami yami vyakula vya aina mbali mbali na hapa ameniambia kapika mwenyewe akisaidiana na wifi yake. Anasema kwa kule New York huwa wanatumia sana vitabu vya mapishi na chakula kinatoka vizuri, ila huku sie mara nyingi twaita watu wa cartering watusaidie, tujifunze kutoka kwake, vitabu vya mapishi vipo haapa kwetu kwenye maduka ya vitabu na kama utakuwa huna muda wa kwenda kununua, basi, kwenye hii blog yangu kuna icon imeandikwa cook it, angalia inakuelekeza kitu chochote ukitakacho kupika, sijaweka kama urembo, tumieni itawasaidia sana.


Tuesday, December 1, 2009

Ukimya huu wa siku moja sio wa bureeee!!!!!!!!!!

Naomba kuchukua fursa hii kwa ukimya wangu kuwaomba radhi, ila sio wa bure, nina suprise nilikuwa nikiwaandalia.

Tuonane tena kesho kwenye blog yetuuuu

Siku njema...

Hata vitambaa vyepesi vyafaa pia


Aina za net na urembo wake