Monday, September 7, 2009

Garden


Nimeombwa kuelezea garden na mmoja wa mdau mwenzetu, wengi tunapenda sanaaa garden zetu, ila kuanza na mahali gani iwe ndio inakuwa ni matatizo. Garden inahitaji uangalizi wa karibu sanaaa na usiwe bahili wa hela, na cha kuangalia baada ya kuamua kuanzisha garden ni:

  • Kwanza ujue udongo wako ni wa aina gani
  • Kuna maji ya kutosha
  • Eneo lako lina ukubwa kiasi gani
  • Hali ya hewa pia e.g. joto ama baridi
  • Kuna miti mikubwa
  • Nyumba yako iko eneo gani kwa jinsi ulivyoijenga  (pembeni, katikati, nyumba, ama mbele ndani ya fensi)

Sasa ukisha gundua hili, itakusaidia kujua upande maua aina gani, mpangilio gani na style ipi. 

Mahitaji ya kuanzisha garden ni:

  • Jembe
  • Beleshi
  • Wheel baro
  • Reki
  • Mbolea 
  • Kamba
  • Mkasi
  • Gloves
  • Overroll
  • Buti za plastic
  • Udongo (huu udongo hununuliwa una rangi kama nyekundu hivi ama mweusi mweusi) kwa ajili ya kuchanganyia wakati ukiandaa maua kwa ajili ya kupanda)
  • Maji
  • Maua
  • Madawa ya kuua wadudu

Maua yako ya aina nyingi sanaaaa. Kwa hiyo kua mwangalifu sanaaa wakati wa kununua maua kwa ajili ya kupanda kwenye garden yako chagua maua yanayolingana na hali ya hewa uliyopo. kama vile joto, baridi etc.

Maua ya kwenye vyungu, pia udongo, uwe umechangwanywa vizuri na mbolea, ua lilingane na chungu sio chungu kidogo ua kubwa, na yasikae sana juani, tafuta sehemu yenye jua la wastani, na kama unayaingiza ndani basi kila baada ya siku nne mpaka tano litoe nje lipate mwanga, bila kufanya hivyo litakufa. 

Maua yote haya yanahitaji kupapaliliwa. Na hakikisha maua yamwagiliwa kwa siku mara mbili. Maua ya liyopandwa kwenye vyungu yamwagiliwe maji kidogo, ukiweka mengi yataoza.

Friday, September 4, 2009

Comments

Ndugu wadau asante kwa comments zenu kwani mnanisaidia sanaa. Naomba kuwahakikishia kuwa ninazifanyia kazi comments zenu, na msiache kuniletea aidia zenu, kwa kufanya hivi tutakuwa tunasaidiana sanaaa.

Hii blog ndio kwanza imeanza na nina mikakati mingi kweli ya kutusaidia mazingira yetu, kwa sasa kuna program naziandaa zikiwa tayari nitawajulisha ila kwa dondoo ya baadhi ya hizo program, niko mbioni kuanzisha services za:

  1. Kutengeneza garden na kuihudumia
  2. Kudecorate nyumba
  3. Kupamba sherehe mbali mbali
  4. Kua arrange furnitures majumbani na maofisini.

Hayo ni baadhi tuu ya mambo ninayopanga kuyafanya, inahitaji kujipanga vizuri ili nisije nika waboa wadau wangu, na vitu vizuri havihitaji haraka. Endeleeni kuniletea maoni ya nini kifanyike nami nitakifanyia kazi. KWANGU HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KWA HUU UPANDE WA HOMES DECORATIONS.

Shukrani kwa funs wangu woteeeeee!!!!

eti wadau nianzishe hii service ya kupanga nguo ama?



Jinsi ya kupanga nguo kabatini

Nashukuru sana kwa maoni yenu. Na naomba msisite kuniandikia kitu gani niwaeleweshe. Kama mdau wangu hapa ambaye anataka kujua jinsi ya kuhifadhi nguo kabatini.

Neno la kwanza  tukienda kwenye makabati yetu kuchukua nguo ya kuvaa utasikia sioni nguo, ama sina nguo wakati kabati limejaa nguo. Na hii ni kutokana na  mpangilio mbaya wa nguo,  na ndio maana tumekuwa tukirudia rudia nguo mara kwa mara kwa kujua ama bila kujua. Na wanaoongoza kwa nguo nyingi duniani ni wanawake. Utakuta mtu ana nguo nyingi na anazo zivaa ni chache, na hii hutokana na kwamba hana mpangilio mzuri wa nguo zake. Hakikisha kwamba kabla hujaanza kupanga chagua nguo usizozivaa zitowe, na uzigawe kwani itakusaidia kupata nafasi na kujua ukienda kufanya shopping ununue zipi. Ziko stepu kama nne ama tano ya kupanga nguo.

  • Panga nguo kwa misimu kwa wale walio sehemu za baridi
  • Panga nguo kwa types za nguo, kama unaona kupanga kwa misimu kwako haiwezekani, basi kuna njia hii ya pili, nikizungumzia types ni kama, mashati, tishet, sketi, suruali etc. kwa njia hii itakusaidia kujua ni nguo za aina gani unazo, na pia itakusaidia kuchagua nguo kwa urahisi, na kujua idadi.
  • Panga nguo kwa rangi, hii itakusaidia pia kuchagua nguo zinazoendana kwa urahisi, mfano kama una tisheti ya pink na umeitoa sehemu uliyopanga tisheti peke yake kwa rangi,  utaenda ulipopanga sketi, na itakuwa ni rahisi kujua ni rangi gani uchague inayoendana na tisheti ile.

  • Kupanga nguo zilizokunjwa, sasa kuna kupanga kwa aina mbili kama kabatini basi panga pia kwa rangi na kwa kuzilaza kama tulivyozoea, ila kama ni kwenye droo basi panga kwa rangi pia ila kwa kuzisimamisha kama ilavyoonekana hapa.

Thursday, September 3, 2009

Ofisi za ndani ya nyumba











Sio wote wameajiriwa,  wengine wamejiajiri, sasa basi nimejitahidi kuonyesha jinsi ya kudizaini ofisi ndani ya nyumba yako. Na hii inatokana na nafasi ya nyumba yako.

Wednesday, September 2, 2009

Hata chooni mapazia yanahitajika




Hili pazia lingekaa jikoni kwako ingekuaje?








Leo nimeamua kurudi tena eneo la jikoni, haya mapazia ni rahisi kutengenezwa na yanapatikana. Ni mazuri.