3d ni michoro ambayo huchorwa kwa kutumia computer na software maalum, ili kuweza kuona ni jinsi gani jengo lako itakua tayari baada ya kujengwa, na muonekano wake kwa ujumla, mpangilio wa fanicha ndani, na kuweza kukuonyesha makosa madogo na makubwa......
Hapa chini ni baadhi ya michoro ya 3d, ambapo tumeweza kuonyesha mfano wa nyumba itakavyoonekana baada ya kwisha kujengwa kwa nje....
3d yaweza kua niya garden, ya nyumba nje, ya mpangilio ndani, etc....ni wewe mwenyewe unahitaji nini.....
Katika kazi yangu hii nimekua nikikutana na makosa mbali mbali ambayo wateja wangu wamekua wakiyalalamikia, kwamba jiko limekua ni dogo, ama chumba kidogo. ama hakutaka muelekeo huo.....mara vipimo havieleweki, rangi sio nzuri.......mpangilio wa fanicha. vitu haviendani. switch za umeme hazikuaa sehemu husika...etc.....ni tatizo kwa kweli......
Kitu kingine nimegundua kua katika ujenzi wa nyumba zetu, hua hatuna ule utaratibu wa kua wawazi kwa archtects(wachora ramani). Hausemi nini unataka, yaani we umeona nyumba ya flan basi unataka kua kama na yake na inabadilishwa kidogo tuuuu.......(copy and paste).
Jamni designs za nyumba ziko nyingi mno.....na ndio maana utakuta hapa kwetu nyumba zinafanana mno.......ukiona nyumba imebadilika basi ujue hiyo nyumba mwenye hakai sana hapa, kaja na mchoro wake toka nje.....
(nitalizungumzia hili siku ingine kwenye mada yake) inafika kipindi tuambizane ukweli....sasa......(let's be creative)
kwa upande wa 3d, kama tungekua tunafuatilia ama kujua mapema, wengi wetu tusingekumbana na matatizo haya....maana saa ingine utakuta ukuta umezidi, inabidi kubomoa.......sasa hizo ni gharama zisizokua na maana.......