Wednesday, December 1, 2010

She is always envromental friendly, Hii ni miji ya wenzetu, ona beach zao zilivyo nzuri na safi.....Yaani hapa nilipiga picha akilini mwangu baada ya kutumiwa picha na Jossyanne, pale coco beach, lol, ingekuwa kama hivi si ingependeza jamani?

Tuyatunze mazingira na kuyalinda mazingira nayo yatatulinda siku zote, wanamazingira wa Tanzania mazingira yapewe kipaumbele kikubwa ktk jamii yetu na tukishirikiana tunaweza, kuanzia ngazi ya familia, kaya jamii mashuleni vyuoni mpaka taifa, sehemu za biashara maofsini nk.

Napenda sana kulinda mazingira na kuyatunza, tukishirikiana tunaweza siku zote umoja ni nguvu. watanzania wenzangu tuone aibu miji ya wenzetu ni misafi ina mpangilio mzuri kwanini sisi tushindwe? tunasafiri kila mara, tuna macho tunaona kwanini hatupendi kuiga mazuri tukayafanya nchini kwetu? ninaamini tukiamua tunaweza. sana asanteni .  

Sorry for my silence,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataka radhi wadau wangu wotee, kwa kuwa kimya, as I am approching my last trimester.

Nawakumbuka sana na nawapenda sanaaaaa.